Unknown Unknown Author
Title: Kizimbani kwa kukutwa na nyara za serikali
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WAKAZI wastatu wa Kijiji cha Ninde mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa wamefikishwa katika Mahakama ya Wila...

WAKAZI wastatu wa Kijiji cha Ninde mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi kwa kosa la kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh 900,000.
Washitakiwa hao Joseph Julio (60), Salvatory Lyambise (58) na Datus Kanondo (38), walifikishwa jana mbele ya Hakimu Lilian Lutahangwa ambako walikanusha mashtaka yao.
Awali Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Hamim Gwelo alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 30, 2016 usiku wa manane.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa usiku huo wa tukio washtakiwa hao walikuwa wakiwa na pembe za mnyama aitwae insha na nyama ya mbawala kinyume cha sheria.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top