Unknown Unknown Author
Title: Serikali kusaidia wawekezaji wadogo wa kuzalisha umeme
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Nishat Profesa Sospeter muhongo SERIKALI ya Tanzania itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali amba...
Waziri wa Nishat Profesa Sospeter muhongo
SERIKALI ya Tanzania itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ambayo wananchi wameamua kuiendeleza, ikiwemo miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali kama maji, upepo, jua, nishati jadidifu, makaa ya mawe na mawimbi ya bahari.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa kikao chake na wazalishaji wa umeme wa maji na wale wanaotaka kuzalisha umeme huo chini ya megawati 20 kilichofanyika katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Mtera.
“Serikali lazima iwe msemaji wa wawekezaji hawa ili kuhakikisha wanapata fedha na teknolojia za kuendesha miradi yao na hii itapelekea Taifa kuwa na nishati ya kutosha kwani wawekezaji hawa sasa watakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme,” alisema Profesa Muhongo.
Ili kufanikisha suala, Profesa Muhongo aliwataka wadau hao wanaotaka kuzalisha umeme wa maji chini ya megawati 20 kuhakikisha kuwa wanaandika na kuwasilisha wizarani mapendekezo yanayochanganua miradi wanayotaka kuanzisha kabla ya mwisho wa mwezi huu ili litengenezwe kabrasha moja litakalotumika katika kuombea fedha kwa wafadhili mbalimbali na taasisi za kifedha.
“Ifikapo tarehe 28 mwezi huu mchanganuo wa mapendekezo yenu yawe yamemfikia Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati ili serikali iangalie namna ya kutafuta fedha zitakazowawezehsa kuendeleza miradi yenu ya umeme badala ya mtu mmoja mmoja kuanza kuzunguka na maombi yake binafsi ya kutafuta fedha kutoka taasisi mbalimbali jambo linalochelewesha upatikanaji wa fedha hizo,” alieleza Profesa Muhongo.
Profesa Muhongo alisema tayari serikali imeshaanza majadiliano na taasisi za kifedha kama Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Dunia (WB) na nchi wahisani ili kupata fedha za kuendeshea miradi ikiwemo ya nishati.
Alisema suala hilo litafanyika kwa ufanisi endapo miradi yote inayoombewa fedha itajumuishwa katika kabrasha moja litakaloainisha miradi yote inayohitaji kuendelezwa.
Alisema kwa sasa serikali inazalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo gesi asilimia 50, maji (35%), na mafuta mazito (15%) na kueleza kuwa Tanzania bado ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme vinavyohitaji wawekezaji makini ikiwemo upepo, joto ardhi, makaa ya mawe na jua ili nchi iwe na umeme wa uhakika, unaotabirika na wa bei nafuu.

Source:
Habari Leo

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top