Unknown Unknown Author
Title: Kampuni ya simu kutoa gawio la bilioni 3/-
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa kitengo cha Airtel Money KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza kutoa gawio la faida la zaidi ya Sh bilioni tatu kwa...
Meneja wa kitengo cha Airtel Money
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza kutoa gawio la faida la zaidi ya Sh bilioni tatu kwa wateja wake wa Airtel Money takribani milioni sita pamoja na mawakala wake.
Gawio hilo la faida ni la kipindi cha kuanzia Aprili 2015 hadi Desemba 2015.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo, kila mteja wa Airtel Money atapokea gawio lake kulingana na kiasi cha salio lake katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Meneja wa Kitengo cha Airtel Money, Asupta Naligingwa alisema: “Tunayo furaha kubwa kutangaza mpango wetu wa kugawa faida ya shilingi 3,287,107,061 kwa watumiaji wa huduma yetu ya Airtel Money pamoja na mawakala nchi nzima. Hii ni mara ya pili kwa kampuni yetu kutoa gawio kwa wateja watu, kwani mwaka jana tulitoa kiasi cha jumla ya shilingi bilioni 5.3.”
Meneja huyo alisema kwamba wanaamini gawio hilo litaleta tija kwa wateja wetu na hivyo kudhihirisha dhamira yao ya kutoa huduma bora za kifedha nchini.
Huduma ya Airtel Money inawawezesha wateja kulipia ankara za huduma na bidhaa, kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi vya data, kutuma na kupokea fedha, kutoa fedha kwenye akaunti zao za Airtel Money, kutoa na kutuma fedha kutoka kwenye akaunti zao za benki na nyingine nyingi.
Aidha, Airtel Money kupitia huduma ya Airtel Timiza imeendelea pia kuwa huduma ya kibunifu na ya kuigwa kwa kutoa mikopo ya haraka, isiyo na dhamana kwa wateja na mawakala wa Airtel Money nchini.

Source:
Habari leo

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top