![]() |
| Wakili wa Ruto Karim Khan |
Kesi ya uhalifu inayomkabili naibu
rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu
wa kivita ya The Hague hatimaye imeanza.
Ruto yuko katika mahakama
hiyo na mwandishi Joshua Arap Sang ambaye pia anajaribu kutoa ushahidi
utakaosababisha kufutiliwa mbali kwa kesi hiyo inayohusishwa na ghasia
za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.Mnamo mwezi Disemba mwaka jana mahakama hiyo ilifutilia mbali mashtaka dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa ukosefu wa ushahidi,lakini mwendesha mashtaka anahoji kwamba bwana Ruto na mwandishi Joshua Sang wana kesi ya kujibu.
Washtakiwa wanasema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea huku wakikana mashtaka hayo.

Post a Comment Blogger Facebook