![]() |
| Mgombea ubunge wa Songea Mjini, CCM, Leonidas Gama. |
Gama aliyasema hayo juzi, wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika mtaa wa Mkwepu na kusisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi na wagombea wake wa udiwani, ubunge na rais ndicho chenye sera madhubuti inayotekelezeka katika kuwaondolea umaskini wakazi hao.
Mbali na hilo, Gama aliwaomba wananchi hao kuacha kuwajaribu kwa kuwapa uongozi upinzani kwa sababu wana tabia ya kurudisha nyuma maendeleo kila wanapopata nafasi ya uongozi kutokana na tabia yao ya kupinga kila kinachofanywa na Serikali ya CCM.
Alisema iwapo wananchi wa Songea watampa ridhaa ya kuwa Mbunge wao moja kati ya vitu atakavyosimamia ni kupigania kurudisha heshima ya wakulima ili kuwa na soko la uhakika kwa ajili ya kuuzia mazao.
Alisema yeye anatambua majukumu yake, kwa kuwa ni kiongozi anayejua kero za Wananchi kwa hiyo kama watamchagua kuwa Mbunge wao atayashawishi kampuni kubwa za ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza hatua itakayosaidia watu wengi kupata ajira.

Post a Comment Blogger Facebook