Unknown Unknown Author
Title: WATENDAJI WA TANESCO KUFUTWA KAZI NA RAISI HUYU ATAKAE KUA KATIKA AWAMU YA 5
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya watendaji wa Tanesco Kufutwa kazi rasmi baada ya kuapishwa rais wa serikali ya awamu ya 5, siku chache baada ya zoezi la ku...

Baadhi ya watendaji wa Tanesco Kufutwa kazi rasmi baada ya kuapishwa rais wa serikali ya

awamu ya 5, siku chache baada ya zoezi la kupiga kura na kumtangaza mshindi.


hilo limebainika baada ya wagombea wenye ngvu zaidi, Edward lowassa wa Chadema na Dk. John Magufuli
wa CCM kuweka wazi kwa nyakati tofauti kua endapo watachaguliwa kuingia ikulu watawafuta kazi baadhi
ya watendaji wa Tanesco kwa kile walichodai kua ni uzembe unaopelekea kua tatizo la ukosefu wa umeme
nchini.

Akiongea katika mkutano wa kampeni jijini Arusha, Dk Magufuli aliahidi kuwa kuingia tatizo la umeme
chini litakua la kihistoria lakini ataanza na watendaji ikiwa ni pamoja na Mawaziri.

"Najua mawaziri wapo kwenye kampeni lakini nao wajiandae zimebaki siku 18,"alisema Dr. Magufuli.

kwa upande wa Edward lowassa, akiwa katika harakati zake za kampeni mkoani kilimanjaro,aliahidi
kua atahakikisha atamaliza tatizo la umeme chini kwakua hio ni nishati muhimu inayochangia kwa
asilimia kubwa katika uchumi wa nchi.

pia,aliwataka baadhi ya watendaji wa shirika hilo la umeme nchini kujiandaa kuondoka katika nafasi zao
kwa kushindwa kulitatua tatizo la umeme na kukata umeme pasipokua na sababu za msingi.

"nasikitika hali ya umeme nchini, kila siku wanakata umeme na maelezo hayatoshelezi. Na mara nyengine
hawatoi maelezo, wanatuacha tu. Kila mtu anapata adha na tabu bila ya sababu. Kila siku umeme unakatika
mara 3 mara 4, nauliza serikali iko wapi? Kwanini hawa wanaosema uongo hawajibishwi?"Lowassa alihoji.

"Serikali nitakayo iongoza mimi,mtu akinifanyia mchezo wa namna hiyo namfukuza kazi mara moja,
apo apo. Uchumi unasimama kwa kukosekana umeme wa uhakika, uwezo upo lakini viongozi wetu wameshindwa
kulitatua . Ninawambia Tanesco wajipange,baadhi ya watendaji watafute kazi nyengine,"Alisema Lowassa.

Kwa kipindi cha takribani siku 5, nchi imekumbwa na tatizo la mgao wa umeme ikiwa ni siku chache uongozi
wa Tanesco utangaze kua tatizo hilo litakua historia ikiwa tayari wmekwisha unga umeme huo katika mfumo
wa Gesi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top