![]() |
Burka |
Mwanachama mwandamizi wa chama cha
kikomyunisti katika jimbo la Xinjiang amesema kuwa vazi la kufunika uso
la Burqa sio la kiislamu bali ni la itikadi kali.
Afisa huyo
alitoa matamshi yake katika hafla ya maendeleo katika jimbo hilo,ambalo
ni makaazi ya waislamu wasio wengi wa kabila la Uighur.Serikali imeweka marufuku ya nguo za kidini katika jimbo la Xinjiang,ambapo inalaumu waislamu wanaotaka kujitenga kwa ghasia zilizosababisha vifo vya watu wengi katika kipindi cha miaka michache iliopita.

Post a Comment Blogger Facebook