Unknown Unknown Author
Title: Makumbusho ya wanajeshi wa Ujerumani na Ufaransa yafanyika
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Sherehe za miaka 100 za kuwakumbuka wanajeshi wa Ujerumani na Ufaransa waliouwawa wakati wa vita vikali vya muda mrefu enzi ya vita ...

Sherehe za miaka 100 za kuwakumbuka wanajeshi wa Ujerumani na Ufaransa waliouwawa wakati wa vita vikali vya muda mrefu enzi ya vita vikuu mwaka 1916 zinafanyika kaskazini mwa Ufaransa.

Sherehe hizo zilianza na hotuba kutoka kwa kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na mwenyeji wake wa Ufaransa, Francois Hollande.
Angela Merkel na Francois Hollande wakiweka maua.
Wote wawili waliweka shada za maua katika makaburi ya wanajeshi hao huko Consenvoye.
Zaidi ya wanajeshi laki tatu wa Ufaransa na Ujerumani waliuwawa katika makabiliano hayo, yaliyofanyika kaskazini mashariki mwa Ufaransa kwa zaidi ya miezi tisa mnamo mwaka 1916.


About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top