Unknown Unknown Author
Title: China yazuia meli za Korea Kaskazini
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meli za ulinzi wa pwani ya China China imepiga marufuku meli za Korea kaskazini kuingia katika bandari zake kuanzia hivi leo. Waziri ...
Meli za ulinzi wa pwani ya China
China imepiga marufuku meli za Korea kaskazini kuingia katika bandari zake kuanzia hivi leo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa china ameripotiwa kutangaza vikwazo hivyo katika mkutano wa kila mwaka wa maafisa wa chama cha kikomunisti mjini Beijing.
Hatua hiyo inaileta China sambamba na vikwazo vikali vilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini wiki iliyopita.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un

Japan nayo imetoa malalamishi kwa korea kaskazini kufuatia hatua yake ya kurusha makombora ya masafa mafupi mashariki mwa pwani ya nchi hiyo.
Siku ya Jumanne kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema kuwa nchi yake imeunda zana za kinuklia zinazoweza kutundikwa kwenye makombora ya masafa marefu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top