Unknown Unknown Author
Title: Murray,Konta watinga robo fainali
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Johanna Konta Nyota Johanna Konta amekua mchezaji wa kwanza wa kike wa Uingereza kufanikiwa kutinga hatua ya robo ya Grand Slam ikiwa ...
Johanna Konta
Nyota Johanna Konta amekua mchezaji wa kwanza wa kike wa Uingereza kufanikiwa kutinga hatua ya robo ya Grand Slam ikiwa ni miaka 32 toka alipofanya hivyo Jo Durie.
Konta alipata ushindi dhidi ya Mrusi Ekaterina Makarova kwa jumla ya seti 4-6 6-4 8-6, Mwingereza wa mwisho kufika robo fainali ya Grand Slam alikue ni Jo Durie, aliyefika hatua hiyo katika michuano ya Wimbledon ya mwaka 1984.
Nae Andy Murray akasonga mbele kwenye hatua ya nane bora kwa kumshinda mpinzani wake Bernard Tomic.
Murray alipata ushindi wa seti 6-4 6-4 7-6 (7-4).Hatua ya robo fainali kwa upande wa wanaume itawakutanisha
Novak Djokovic na Kei Nishikori Roger Federer na Tomas Berdych
Gaels Monfils na Milos Raonic David Ferrer na Andy Murray
Robo fainali kwa upande wa wanawake
Serena Williams na Maria Sharapova, Agnieszka Radwanska na Carla Suarez Navarro
Angelique Kerber na Victoria Azarenka ,Johanna Konta na Shuai Zhang

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top