Saudi Arabia imekana ripoti kuwa
mkanyagano uliowaua zaidi ya watu 700 karibu na mji wa Mecca
ulisababishwa na kufungwa kwa barabara ili kuruhusu watu mashuhuri
kuingia eneo hilo.
Wizara ya masuala ya ndani ilisema kuwa madai
hayo ni ya uongo na kwamba uvumi huo ulianzishwa na vyombo vya serikali
Iran ambayo ilipoteza raia 131.Iran imeilaumu Saudi Arabia kwa mkasa na ikataka wahusika wote kuchukuliwa hatua za kisheria.

Post a Comment Blogger Facebook