![]() |
| Dalili za mapatano Burkina Faso |
Wapatanishi wa Afrika wanasema kuwa wanakaribia kumaliza mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso.
Viongozi hao wa mataifa ya Afrika Magharibi wanasema kuwa mazungumzo yao yanalenga kurejeshwa kwa utawala wa kiraia wa mpwito.Rais wa Benin, Yayi Bon, anasema kwa kuna uwezekano mkubwa kuwa viongozi wa wa mapinduzi hayo wako tayari kumuachilia rais Michel Kafando kutoka kizuizi cha nyumbani na kumrudish mamlakani.
Mazungumzo yamekuwa yakifanyika katika mji mkuu Ouagadougou baada ya siku ya tatu ya maandamano ya kupinga mapinduzi ya rais Kafando yaliyofanywa na kikosi cha kumlinda rais.
Akiongea na kiongozi wa mapinduzi hayo, jenerali Gilbert Diendere, rais wa Benin anasema kuwa anatarajia kile alichokitaja kuwa habari njema kutangazwa baadaye leo Jumapili.
![]() |
| Watu kumi wamepoteza maisha yao huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa |
![]() |
| Haijabainika hadi kufikia sasa kiongozi wa mapinduzi haya Gilbert Diendere atatoa masharti yepi |
Waandamanaji wanamtaka rais wa kipindi cha mpwito Kafondo kuendelea kushikilia hatamu hadi pale uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba utakapomalizika.
Haijabainika hadi kufikia sasa kiongozi wa mapinduzi haya atatoa masharti yepi ya kurejesha mamalaka kwa rais Kafondo na utawala wake.




Post a Comment Blogger Facebook