Unknown Unknown Author
Title: NEC yapata ugeni wa dunia ,Taasisi ya Tume za Uchaguzi Duniani (AWEB)
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani UJUMBE kutoka Taasisi ya Tume za Uchaguzi Duniani (AWEB) umeitembelea Tume ya...
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC,
Kailima Ramadhani


UJUMBE kutoka Taasisi ya Tume za Uchaguzi Duniani (AWEB) umeitembelea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kujifunza hatua mbalimbali zinazofanywa na NEC wakati wa uchaguzi nchini.

Aidha, ujumbe huo umekuja na aina mpya ya teknolojia ambayo ina uwezo wa kuandikisha wapiga kura, kutuma taarifa za wapiga kura katika kanzidata kutoka katika kituo cha kujiandikishia na kuhakiki wapiga kura siku ya uchaguzi.
Mashine hiyo ambayo ni ndogo ukilinganisha na ile ya Biometric Voter Registration (BVR) ina uwezo wa kutumiwa na mtu mmoja ambaye ataweza kuandikisha mpiga kura katika hatua zote hadi kupata kitambulisho cha mpigakura na inabebeka kirahisi.
Teknolojia hiyo mpya pia inaweza kurahisisha utendaji kazi katika masuala ya uandikishaji wapiga kura, kuhakiki wapiga kura na kutuma taarifa katika kanzidata.
Ujumbe wa AWEB kwa NEC umeongozwa na Mkurugenzi wa Mipango na Operesheni Lee Ju-Hwan, Mtafiti Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi, Park Jae Sumg.
Ujumbe huo umekutana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani na kufanya mazungumzo naye ofisini kwake baada ya kukutana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya tume hiyo, kutembelea ofisi mbalimbali za tume hiyo na kujifunza.
Akizungumzia ujio wao jana jijini Dar es Salaam, Ju-Hwan alisema yeye na ujumbe wake wamekuja kubadilishana uzoefu katika teknolojia ya kuandikisha wapiga kura.

About Author

Advertisement

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment Blogger

 
Top