Unknown Unknown Author
Title: Mchezaji wa Newcastle United ahukumiwa na kutakiwa heri
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Cisse alikivunja sheria ya leseni za udereva Mchezaji nyota wa klabu ya Newcastle United ya Uingereza amepigwa faini na hakimu na kisha...
Cisse alikivunja sheria ya leseni za udereva
Mchezaji nyota wa klabu ya Newcastle United ya Uingereza amepigwa faini na hakimu na kisha akatakiwa heri katika Ligi ya Premia.
Mshambuliaji Papiss Cisse, kutoka Senegal, aliadhibiwa baada ya kupatikana na kosa la trafiki.
Alikuwa amepewa leseni ya kuendesha magari mwaka mmoja nchini Uingereza lakini amekuwa akitumia leseni hiyo kwa miaka mitatu.
Cisse, 30, anayeishi Darras Hall, Ponteland, alipewa alama nne na akapigwa faini £547 na mahakimu Newcastle.
Klabu yake inakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja katika Ligi Kuu ya England na baada ya kumsomea hukumu, mwenyekiti wa jopo la mahakimu Carolyn Hyslop kisha alimwambia: "Kila la kheri kesho."
Newcastle wamo hatarini ya kushushwa daraja
 Newcastle United watakutana na Swansea City uwanjani St James' Park Jumamosi kwenye mechi ambayo wanahitajika kushinda kujiongezea matumaini ya kunusurika.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top