![]() |
| Waasi wenye msimamo mkali wa kidini wa Abu Sayyaf wamewaua wanajeshi 18 Ufilipino |
Jeshi la Ufilipino limekiri kuwa
wanajeshi 18 wameuawa katika makabiliano makali na wapiganaji waasi wa
Abu Sayyaf Kusini mwa taifa hilo.
Limeongeza kuwa wanajeshi wengine 50 walijeruhiwa wakati wa makabiliano katika kisiwa cha Basilan.Wapiganaji watano wa kundi hilo la Waislamu wenye itikadi kali waliuawa.
Inasemekana wanajeshi walikuwa wakimlenga kamanda wa Abu Sayyaf Isinilon Hapilon, ambaye ameapa uaminifu wake kwa kundi la Islamic State.
![]() |
| Kamanda wa Abu Sayyaf Isinilon Hapilon,ameapa uaminifu wake kwa kundi la Islamic State. |
Serikali ya Marekani imetangaza zawadi ya dola milioni 5 kwa habari zozote zitakazosaidia kumtia mbaroni Hapilon.


Post a Comment Blogger Facebook