Unknown Unknown Author
Title: Magufuli ahakiki bunduki zake mbili
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais Magufuli akiitoa bastola yake ihakikiwe Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa bunduki zake mbili aina ya shortgun na pistol ...
Rais Magufuli akiitoa bastola yake ihakikiwe
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa bunduki zake mbili aina ya shortgun na pistol na zikahakikiwa nyumbani kwake ikulu jijini Dar es salaam.
Kiongozi huyo ndiye mtu kwanza kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam la kuhakiki silaha, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Uhakiki wa silaha hizo umefanywa na maafisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Rais Magufuli ametoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha nchini humo kuhakikisha zinahakikiwa.
Aidha, amelitaka jeshi la polisi kuongeza juhudi za kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.
"Ni aibu kumuona askari polisi mwenye silaha ananyang'anywa silaha, ni aibu, na nasema hiyo ni aibu, mpaka jambazi akunyang'anye silaha na wewe una silaha?" amesema Dkt Magufuli.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top