![]() |
| Shambulizi la bomu laua watu 50 Iraq |
Takriban watu 50 wameuawa katika mji
wa Hillah Iraq baada ya mlipuaji wa kujitolea mhanga kulipua lori
lililokuwa limejazwa vilipuzi.
Lori hilo la kubeba mafuta
lilisogezwa karibu kabisa na kituo cha kupekulia magari nje ya mji mkuu
wa Baghdad kabla ya kujilipua.39 ya wale waliouawa walikuwa ni raia huku waliosalia wakiwa ni polisi.
![]() |
| 39 ya wale waliouawa walikuwa ni raia huku waliosalia wakiwa ni polisi. |
Shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa 9 asubuhi saa za mashariki ya kati.
Watu wengi zaidi walijeruhiwa.
Wakuu wanasema lori lilokuwa na mabomu, liliripuka, na kusababisha vifo, kati ya magari mengi yaliyokuwa yakisubiri kupekuliwa.
![]() |
| Mji wa Hill uko kilomita mia moja kusini mwa Baghdad. |
Mji wa Hill uko kilomita mia moja kusini mwa Baghdad.
Kundi la wapiganaji la Islamic State limedai kutekeleza shambulizi hilo kupitia mtandao wake wa Amaq.



Post a Comment Blogger Facebook