Unknown Unknown Author
Title: Mwinyi Kazimoto wa Simba afikishwa kituo cha polisi Shinyanga, kisa mwandishi wa habari
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
February 10 stori kutoka  Shinyanga  walikoweka kambi timu ya wekundu wa Msimbazi Simba  wakisubiri mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya klab...
February 10 stori kutoka Shinyanga walikoweka kambi timu ya wekundu wa MsimbaziSimba wakisubiri mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya klabu ya Stand United, zimeandikwa stori mpya kuhusu kiungo wa timu hiyo kufikishwa kituo cha polisi, kiungo wa SimbaMwinyi Kazimoto ameripotiwa kufikishwa kituo kikuu cha polisi Shinyanga.
Mwinyi Kazimoto amefikishwa kituo kikuu cha polisi mkoani Shinyanga, kwa tuhuma za kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti la MwanaSpoti Mwanahiba Richard, Kazimotoanayedaiwa kufanya kosa hilo kutokana na kudai kuwa mwandishi huyo aliwaandika vibaya kuwa wachezaji wa Simba waliocheza mechi ya Prisons na Mbeya City walikuwa chini ya kiwango na wanapaswa wachunguzwe kwa maana ya kuwa wamepewa rushwa.
Mwanahiba Richard
Hivyo baada ya mazoezi ya Simba yaliofanyika uwanja wa Kambarage mkoaniShinyanga ndio inaripotiwa Kazimoto alitenda kosa hilo, bado Kazimoto na viongozi waSimba hawajapatikana kuzungumzia chochote juu ya tuhuma hizo,  Mwanahiba aliriripoti katika kituo cha polisi na kupewa hati ya mashitaka (RB) yenye nambaSHY/RB/895/2016, fomu ya matibabu (PF3) kisha akapelekwa hospitali kwa matibabu.
CHANZO CHA STORI HII: Salehjembe

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top