Maafisa wa Marekani wamethibitisha kuwa ni ndege za Marekani zilizofanya mashambulio huko Libya wakiwalenga wanamgambo wa IS.
Hata
hivyo shambulio hilo la karibu na mji wa Sabratha,lililonuiwa kumlenga
hasa mpiganaji mmoja wa Tunisia limeripotiwa kuwauwa watu 30 .Mpiganaji huyo wa Tunisia anasemekana ndiye aliyefanya shambulio la mwaka jana katika kumbukumbu za Bardo na hoteli ya ufuoni mwa bahari ya Sousse huko Tunisia ambako watu zaidi ya 10 waliuawa.
![]() |
| Mshambulizi ya ndege za Marekani |
Noureddine Chouchane anahusishwa na mashambulio mawili nchini Tunisia mwaka uliopita ,ikiwemo shambulio lililowaua raia 30 wa Uingereza.
Kundi la IS limekuwa likifanya oparesheni zake nchini Libya kwa kipindi cha mwaka mmoja na Marekani inakadiria kwamba lina hadi wapiganaji 6,000 nchini humo.
![]() |
| Wapiganaji wa Islamic State |


Post a Comment Blogger Facebook