Mechi kati ya viongozi wa ligi ya Uingereza Leicester City dhidi ya Manchester City ambao wako katika nafasi ya pili katika jedwali la ligi hiyo17.38pm:Na Mechi inakamilika hapa Leicester City wakiibuka kidedea kwa bao 3-1 dhidi ya wenyeji Manchester City.
17.37pm:Lalalal Manchester City wakosa bao la wazi hapa baada ya gusa niguse ya Aguero na Fernando
17.36pm:Baada ya kupata bao la kwanza wachezaji wa Manchester City wanajaribu kila njia hapa kupata bao la pili
![]() |
| Aguero |
17.30pm:Goooooooooooal Aguero aipatia Manchester City bao la kufutia machozi
17.27pm:Mashabiki wa manchester City wanaonekana wakiondoka katika uwanja wao wa Etihad kufuatia mvua hiyo ya mabao
17.26pm: Safu ya mashambulizi ya Manchester City imeshindwa kabisa kuivunja safu ya ulinzi ya Leicester.
17.24pm: Lalalala Verdy akosa bao la nne hapa.Ama kwa kweli ni mvua inyowanyeshea Manchester City
17.21pm:Mahrez naye anatoka kwa upande wa Leicester City
- Gor Mahia imelazwa na Bandari 1-0 katika mechi ya kombe la Gotv mjini Mombasa, kenya
17.20Pm:David Silva atolewa na badala yake Saligno aingia
![]() |
| Kocha wa Leicester Claudio Ranieri |
17.18pm:Hali si hali hapa katika uwanja wa Etihad nchini Uingereza ambapo mabingwa wa zamani wa ligi ya Uingereza Manchester City wameadhibiwa bao tatu bila jibu.
![]() |
| Bao leicester |
17.07pm:Goooooooooooal Leicester City yajipatia bao la tatu dhidi ya Manchester City hapa.Amini usiamini vijana wa Claudio Ranieri wanatamba kama ambaye hawako Etihad
16.57pm:La.la.la.la Manchester City wakosa bao hapa kunako dakika tisa lakini kipa anaukoa.
16.54pm:Wachezaji wa Manchester City hawaamini hapa .Inawabidi kufanya mabadiliko farbian Delph anatoka na badala yake anaingia Fernandinho.
![]() |
| Mahrez |
16.52pm:Gooooooooooal Mahrez wa leicester City aiongezea bao la pili timu yake hapa dakika ya nne baada ya kuanza kwa kipindi cha pili
16.49pm:Na Kipindi cha pili cha mchezo kinaanza hapa katika uwanja wa Etihad.
16.34pm:Na kipindi cha kwanza cha mechi kinakamilika hapa ikiwa wenyeji manchester City wako nyuma kwa bao moja dhidi ya viongozi wa Ligi kwa sasa Leicester City.
![]() |
| Rahim Sterking |
16.33pm:Ama kwa kweli wachezaji hawa wa manchester City wanajaribu kuona lango la wapinzani wao lakini safu ya ulinzi ya Leicester inakaa.
16.32pm:Mechi imekuwa ngumu hapa kwa upande wa Leicester ambao wamerudi nyuma kulinda lango lao.
16.31pm:Dakika za lala salama kpindi cha kwanza, Kolarov anakosa bao hapa
![]() |
| Aguero |
16.30pm:Manchester City inatafuta bao hapa kwa udi na uvumba lakini bahati haijasimama
16.00pm:Ni Mechi inayochezwa huku kukiwa na marasha rasha ya mvua.
15.53pm:Leicester wakosa bao la pili hapa dhidi ya Mancity.
15.50pm:Manchester City Watafuta kusawazisha lakini Aguero ashindwa kuipita safu ya ulinzi ya Leicester.
![]() |
| Leceister |
15.48pm:Goooooooal Leicester City yajipatia bao la kwanza hapa baada mkwaju wa mpira wa adhabu kupigwa,dakika tatu baada ya kuanza kwa mechi
15.45pm: Manchester City vs Leicester City. Mechi inaanza
Kikosi cha Leicester
![]() |
Kikosi cha Man City
|









Post a Comment Blogger Facebook