![]() |
| Majeshi ya Kenya yamekuwa yakikabiliana na wanamgambo wa al-Shabab Somalia tangu 2011 |
Wapiganaji wanaoaminika kuwa wa kundi la al-Shabab wameshambulia kambi moja ya wanajeshi wa Muungano wa Afrika iliyoko kusini mwa Somalia.
Kambi hiyo ya Eel-ade inapatikana takriban kilomita 60 kutoka kwa mji wa Garbaharey, na inatumiwa na majeshi ya Kenya.Majeshi hayo yamo chini ya majeshi ya kulinda amani ya Muungano wa Afrika (Amisom).
Wakazi wa Eel-ade wameambia mwandishi wa BBC mjini Mogadishu kwamba wamesikia milio ya risasi na silaha nyingine kali.
Mapigano bado yanaendelea.
Maelezo zaidi kufuata

Post a Comment Blogger Facebook