![]() |
| Mkutano huo ulikuwa umeitishwa na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby |
Kanisa la Kianglikana duniani limesisitiza kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke na likasimamisha ushirika wa jimbo la Marekani lililotambua ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Jimbo hilo la Marekani, ambalo kwa Kiingereza hujiita Episcopal Church, sasa halitaruhusiwa kushiriki kikamilifu katika masuala ya kanisa hilo.Viongozi wa kanisa la Kianglikana duniani, waliokutana Canterbury, wamesema kanisa hilo lilikiuka Imani inayofuata na waumini wengi wa kanisa la Kianglikana kuhusu ndoa.
Marufuku hiyo ya muda ambayo imepewa jimbo hilo a Marekani inalenga kuzuia kugawanyika kabisa kwa kanisa hilo kutokana na tofauti kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Ndoa hizo zimekuwa zikipingwa sana na majimbo ya kanisa hilo barani Afrika.
![]() |
Gene Robinson ndiye aliyekuwa askofu wa kwanza wa Kianglikana kutangaza hadharani kuwa mpenzi wa jinsia moja mwaka 2003
|


Post a Comment Blogger Facebook