![]() |
| Kisa cha mwisho kiliripotiwa mwezi Novemba mwaka 2015 |
Shirika la afya duniani WHO
limetangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Ebola nchini Liberia na kusema
kuwa maambukizi yote ya ugonjwa huo yamemaliziwa katika eneo la Afrika
Magharibi.
Lakini WHO inasema kuwa bado kazi haijamalizika. Visa
zaidi vinaweza vikaripotiwa na ufuatiliaji wa hali ya juu utahitajika
kuwepo miezi inayokuja.Liberia ilitangazwa kwanza kuwa isiyo na ugonjwa wa Ebola mwezi Mei mwaka 2015 lakini ugonjwa huo ukalipuka tena mara mbili ambapo kisa cha mwisho kiliripotiwa mwezi Novemba mwaka 2015.
![]() |
| Hata hivyo umoja wa mataia umeonya kuwa eneo la afrika magharibi huenda litashuhudia visa vya ungowa wa ebola |
Liberia inajiunga na Guinea pamoja na Sierra Leone ambazo zilipata kutangazwa kutokuwa na ugonjwa huo mwaka uliopita.
Licha ya hilo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, ameonya kuwa eneo la Afrika Magharibi huenda litashuhudia visa vya ungowa huo. Ebola umewaua zaidi ya watu 11,000 tangu mwezi Disemba mwaka 2013 .


Post a Comment Blogger Facebook