Unknown Unknown Author
Title: Apendekeza wakimbizi wapigwe risasi Ujerumani
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Apendekeza wakimbizi wapigwe Risasi ujerumani Mwanasiasa mmoja mbishi nchini Ujerumani ameibua hasira kubwa, baada ya kupendekeza kuwa...
Apendekeza wakimbizi wapigwe Risasi ujerumani
Mwanasiasa mmoja mbishi nchini Ujerumani ameibua hasira kubwa, baada ya kupendekeza kuwa maafisa wa polisi wanafaa kuruhusiwa kuwapiga risasi wahamiaji, wanaojaribu kuingia nchini humo bila idhini.
Kiongozi mkuu wa chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany Frauke Petry, ameliambia gazeti la Mannheimer Morgen, kwamba anapendekeza matumizi ya silaha kwa polisi kama hatua ya mwisho.
Frauke Petry wa chama cha Alternative for Germany

Sheria za polisi wa Ujerumani zinasema kuwa hakuna sheria inayodhinisha kushambulia wakimbizi kwa risasi.
Mwanachama mmoja mkuu wa chama cha Social Democrats, amemkumbusha Frauke Petry kwamba, mwanasiasa wa mwisho wa iliyokuwa Ujerumani mashariki, ambaye alimuru wakimbizi kupigwa risasi, alikuwa Erich Honecker, kiongozi mkuu wa utawala wa kikomunisti ambao ulisambaratika mwaka 1989.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top