Unknown Unknown Author
Title: Alshabaab:Tunawazuilia mateka wa Kenya
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
wapiganaji wa Alshabaab Kundi la wapiganji wa Alshabaab limesema kuwa linazuia kile linachokitaja ni wafungwa wa vita kutoka Kenya k...
wapiganaji wa Alshabaab

Kundi la wapiganji wa Alshabaab limesema kuwa linazuia kile linachokitaja ni wafungwa wa vita kutoka Kenya kufuatia shambulio lao katika kambi ya kijeshi kusini mwa Somalia.
Alshabaab ambao waliivamia kambi hiyo wamesema kuwa wanajeshi 100 wanaohudumu katika muungano wa Afrika waliuawa.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema siku ya ijumaa kwamba baadhi ya wanajeshi wa Kenya waliuawa lakini hakutoa idadi yao.
Al Shabaab wamesema kuwa ni mara ya kwanza kwa kikosi chake cha Saleh Ali Saleh Nabhan kutekeleza shambulio ndani ya Somalia.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Mashambulizi yake mengine yamekuwa nchini Uganda na Kenya.
Saleh Ali Saleh Nabhan alikuwa kiongozi wa kundi la al Qaeda katika eneo la Afrika mashariki ambaye aliuawa katika shambulio la Marekani nchini Somalia mwaka 2009.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top