Unknown Unknown Author
Title: ‘Ufyatulianaji mkali’ wa risasi Paris
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Polisi wamezingira eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis Ufyatulianaji mkali wa risasi u...
Polisi wamezingira eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis
Ufyatulianaji mkali wa risasi umetokea kaskazini mwa Paris katika mtaa wa Saint Denis na ripoti zinasema operesheni ya polisi kuhusiana na mashambulio ya Ijumaa inaendelea.
Maafisa kadha wa polisi wamejruhiwa, kituo cha runinga cha BFMTV cha Ufaransa kimeripoti.
Shirika la habari la AFP lanasema Abaaoud Abdelhamid, anayedaiwa kupanga mashambulio hayo, ndiye aliyekuwa akisakwa kwenye operesheni hiyo mtaa wa Saint Denis.
Afisa mmoja wa polisi amejeruhiwa, mwandishi wa BBC James Longman

Video iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha watu walioshuhudia wakisema milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi unusu alfajiri saa za Ufaransa.
Naibu meya Stephane Peu amewahimiza raia wasalie manyumbani, akisema "hili si shambulio jipya bali ni operesheni ya polisi".
Polisi wamewaondoa raia kutoka eneo hilo

Awali, duru za kiusalama zilisema video ya kiusalama ilikuwa imeonyesha huenda kulikuwa na mshambuliaji wa tisa mashambulio hayo ya Ijumaa.
Watu 129 walifariki kwenye mashambulio yaliyotokea maeneo sita mjini Paris.
Kundi la Islamic State (IS) limesema ndilo lililotekeleza mashambulio hayo.
Ripoti moja inasema barabara zimefungwa eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis.
Uwanja wa taifa wa michezo wa Stade de France, ambako washambuliaji walilipua mabomu Ijumaa, umo kwenye mtaa huo.



About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top