![]() |
| Rais Ma Ying Jeou wa Taiwan (kushoto) na Rais Xi Jin Ping (kulia0 |
Maofisa nchini Taiwan wanasema
kwamba rais wa nchi yao anatarajia kukutana na rais wa China Xi Jin-ping
,Singapore siku ya jumamosi.
Itakuwa ni mara ya kwanza kwa marais wa nchi mbili hizo kukutana ambao hawajawahi kukutana hapo kabla.Wachambuzi wa mambo wanasema huu ndio mwanzo wa kufungua njia ya mahusiano baina ya nchi mbili hizo.
Naye msemaji wa rais wa Taiwan, Ma Ying-jeou,ameelezea lengo la mkutano huo ni kuimarisha amani katika eneo la Taiwani.
Ushirikiano wa nchi hizo umekua zaidi chini ya rais Ma wa chama cha KMT ambaye anaiunga mkono China.
China inaitazama Taiwan kama jimbo lililojitenga ambalo siku moja litarejea kuungana na upande na China.

Post a Comment Blogger Facebook