![]() |
| Bw Kikwete alistaafu baada ya kuongoza Tanzania kwa miaka kumi |
Rais aliyeondoka mamlakani majuzi
nchi Tanzania amesifu jinsi Rais mpya John Magufuli ameanza kufanya kazi
na kumtaka aendelee vivyo hivyo.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete
alisema hayo wakati wa kukabidhi rasmi afisi yake kwa Rais Magufuli
aliyeapishwa Novemba 5 baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu
uliofanyika Oktoba 25.“Umeanza vizuri, baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi,” alisema Bw Kikwete.
Dkt Magufuli amekuwa akifanya ziara za kushtukiza, ya kwanza ikiwa katika makao makuu ya Wizara ya Fedha siku yake ya kwanza kazini ambako aliwakuta wafanyakazi wengi wakiwa wametoka afisini.
Siku chache baadaye, alifanya ziara ya kushtukiza hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alisikitishwa na utoaji huduma.
Hafla ya kukabidhi rasmi afisi kwa Rais Magufuli ilishuhudiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Maafisa wa Ofisi Binafsi ya Rais.
![]() |
| Magufuli alisikitishwa na utoaji huduma Muhimbili na akabadilisha usimamizi wa hospitali hiyo |
Mengine ni hali halisi ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.


Post a Comment Blogger Facebook