![]() |
| Upinzani wapata ushindi mkubwa Poland |
Chama cha Conservative cha Law and Justice cha Poland kimepata ushindi mkubwa zaidi katika uchaguzi mkuu uliofanyika hapo jana.
Ushindi huu ndio mkubwa zaidi kuwahi kupatikana nchini humo tangu mwaka wa 1989.Chama hicho cha Law and Justice kilitumia kibwagizo cha kupambana na uhamiaji na msimamo mkali dhidi ya muungano wa Ulaya kunadi sera zake kwa wapiga kura.
Tathmini ya hivi punde zaidi ya kura zilizopigwa inaonesha kuwa chama hicho cha Law and Justice kimejipatia asilimia 39% ya kura zilizopigwa.
![]() |
| Tayari viongozi wa Law and Justice wameanza kusheherekea ushindi wao Poland |
Chama cha muungano wa vyama wa Civic Platform , Ewa Kopacz, kimekubali kushindwa.
Mwandishi wa BBC aliyeko Warsaw amesema japo taifa hilo limeshuhudia takriban miongo miwili ya ufanisi wenyeji wengi wanadai kuwa hawajafaidika kwa njia yeyote na kujiunga kwa Poland katika muungano wa Ulaya.


Post a Comment Blogger Facebook