![]() |
| Ripoti hiyo imeorodhesha matukio ya utekaji na udhalilishwaji wa wanawake. |
Muungano wa Afrika umeilaumu jeshi
la serikali ya Sudan Kusini na vikosi vya waasi kwa ukiukaji mkubwa wa
haki za binadamu na uhalifu wa kivita.
Uchunguzi wa AU ulibaini
kuwa mapigano yaliyotokea mwezi Disemba mwaka 2013 yalitokana na mzozo
kati ya makabila ya Dinka na Nuer ndani ya kikosi cha kumlinda rais.Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu yao.
![]() |
| Uchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu yao. |
Ripoti hiyo imeorodhesha matukio ya utekaji na udhalilishwaji wa wanawake.
Aidha majina ya watu waliotekeleza matukio hayo imebainika kuwa ni ya raia ambao hawakuwa wakishiriki vita vyenyewe.
![]() |
| Matukio mabaya zaidi yaliripotiwa katika miji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal. |
Matukio mabaya zaidi yaliripotiwa katika miji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal.
Watu kadhaa walioshuhudia mwanzo wa vita hivyo mjini Juba wanasema kuwa walilazimishwa kunywa damu ya watu ambao ndio walikuwa wameuawa.
Makaburi ya halaiki pia yalifichuliwa katika uchunguzi huo ulioendeshwa tangu mwaka jana jopo hilo la uchunguzi lilipoundwa.
![]() |
| Makubaliano baina ya viongozi wakuu yamekiukwa |
Licha ya hofu ya kuwa maelfu ya watu wa kabila fulani walilengwa na kuuawa jopo hilo linasema kuwa Hakukuwa na ushahidi uliopatikana wa kuthibitisha kuwa kulifanyika mauaji ya kimbari.
![]() |
| Miji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal ndio iliyoathirika zaidi |
Watu zaidi ya milioni mbili wamelazimika kutoroka makwao na kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani.





Post a Comment Blogger Facebook