Unknown Unknown Author
Title: MOJA KWA MOJA: YANAYOJIRI UCHAGUZI MKUU TANZANIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
16.55pm: Tume ya uchaguzi nchini Tanzania kupitia mkurugenzi wake imesema kuwa inatarajia kwamba rais mtarajwa atajulikana tarehe 29 huk...

16.55pm:Tume ya uchaguzi nchini Tanzania kupitia mkurugenzi wake imesema kuwa inatarajia kwamba rais mtarajwa atajulikana tarehe 29 huku mipango ya kumpatia cheti cha kuchaguliwa ikifanyika tarehe 30.


16.50pm:Katika kituo cha kupigia kura mjini Dar es Salaam,afisa mmoja wa uchaguzi alionekana akiwapatia raia makaratasi ya kupigia kura ambayo tayari yalikuwa yamewekwa alama ya upigaji kura
Kulingana na mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Kailima Kombo afisa huyo tayari amekamatwa.
Kailima amesema kuwa watakuwa wakitoa matokeo ya uchaguz huo kwa awamu kuanzia hapo kesho saa tatu asubuhi katika jumba la mikutano la Julius Nyerere.

Kailima Kombo mkurugenzi wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania

16.29pm:Huko Rukwa , Magari yaliokuwa yakisafirisha makaratasi ya upigaji kura yalivamiwa na kuchomwa lakini tume ya uchaguzi iliweza kutuma vifaa zaidi asubuhi .
Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania Kailima Kombo amesema kuwa katika maeneo yaliothirika, muda utaongezwa iwapo bado wapiga kura watakuwa katika milolongo.
Amesema kuwa usiku uliopita maafisa waliokuwa wakipewa vifaa vya kupigia kura ,walitaka kuongezwa fedha ikilinganishwa na makubaliano yao.
Hivyobasi walichoma na kuyakata makaratasi ya kupigia kura na kukiwacha kituo hicho bila kitu.Pia walichoma sajili za kupigia kura

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top