Unknown Unknown Author
Title: MOJA KWA MOJA: YANAYOJIRI UCHAGUZI MKUU TANZANIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Bonyeza hapa kupata habari za karibuni zaidi 12.30: Katika kituo cha Meko, nje kidogo ya mji wa Mwanza, kumetokea sokomoko, baadhi ...
Bonyeza hapa kupata habari za karibuni zaidi

12.30:Katika kituo cha Meko, nje kidogo ya mji wa Mwanza, kumetokea sokomoko, baadhi ya wakazi wanalalamika kwamba majina yao hayaonekani kwenye daftari la wapiga kura.
Seif Sharif Hamad
 11.30am:Mgombea wa Urais kupitia chama cha upinzani CUF, Seif Sharif Hamad amepiga kura katika kisiwa kilichopo kisiwani Unguja.
Madereva waliokosa fursa ya kupiga kura
 11.00am:Baadhi ya wapiga kura waliojisajili katika maeneo mengine ya bara wamelazimika kusafiri hadi maeneo hayo ili kupiga kura.Madereva ambao hawakupewa siku ya mapumziko hawafurahii kwamba wasingeweza kushiriki katika shughuli hiyo.
Maguful
10.37am:Mgombea wa Urais kupitia chama cha CCM John Pombe Magufuli amepiga kura katika mkoa wa Kagera huko Chato
Ametoa wito kwa raia wa Tanzania kujitokeza kwa wingi ili kuwachagua viongozi wanaowahitaji.Aidha amewataka raia hao kumtanguliza mungu na kuweka amani.
Anasema kuwa alipopiga kura mvua ilianza kunyesha akisema kuwa ni ishara ya baraka.
Taifa la Ivory Cost
10.15am:Taifa la Ivory Coast linashiriki katika uchaguzi mkuu ulio na ushindani mkubwa ,ikiwa ni wa kwanza kabisa tangu kuisha kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011.Uchaguzi huo umeathirika baada ya wagombea maarufu wa chama cha Upinzani kujiondoa wakidai udanganyifu.
Lowassa
10.00am:Mgombea wa Urais wa chama cha UKAWA Edward Lowassa ameandamana na mkewe katika kituo cha Arusha na kupiga kura
Wanahakiki majina kabla ya kupiga kura

 9.39am:Wakaazi wa Unguja, visiwani Zanzibar, wakihakiki majina, kabla ya kupiga kura.
Dr. Shein
9.36am:Mgombea wa Rais wa CCM, Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein, akiwa katika chumba cha kupiga kura, kusini Unguja.Shein amewataka raia kujitokza kwa wingi ili kushiriki katika shughuli hiyo ya kihistoria.
Milolongo mirefu yashuhudiwa
8.36am:Takriban wapiga kura milioni 22,750,789 wanashiriki katika shughuli hiyo.
Mahame
7.50am:Huku shughuli ya upigaji kura ikiendelea maeneo mengi yamesalia kuwa mahame zikiwemo barabara na maeneo mengi ya mji wa Dar es Salaam.Hii ni kwa sababu raia wengi wanashiriki katika shughuli hiyo.
Amepiga kura
7.14am:Katika kituo cha Dodoma foleni ndefu imeshuhudiwa ,ni kituo kilichopo katikati ya mji.Baadhi ya wapiga kura waliofika kituoni humo na kupiga kura wanasema hakuna tatizo lolote walilopata.
Masanduku yanayotumika kupigia kura Tanzania
7.13am:Katika kituo cha kinondondoni tayari watu wameanza kupiga kura bila matatizo yoyote.Sheria ya mita 200 inaonekana kuanza kuheshimiwa kwani watu wanapiga kura na kuondoka vituoni

7.05am:Mtafarufuku umetokeo katika kituo cha masaki baada ya maafisa wa uchaguzi kutoka nje ya vituo vya kupiga kura na kuwaelezea raia kupanga mistari mitatu inayowapendelea wanawake,na wazee.Wengi wa wale waliofika mapema wamepinga hatua hiyo wakidai kwamba ni haki yao kupiga kura wa kwanza.
WApiga kura
7.00am:Ni saa moja kamili saa za Afrika mashariki na wakati muhimu kwa taifa la Tanzania ambapo shughuli ya upigaji kura inaanza rasmi
Waangalizi
6.30am:Waangalizi wa kimataifa tayari wamefika katika vituo vya kupigia kura katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania ili kushuhudia matukio ya uchaguzi huo.

6.30am: Ili kutaka kufahamu iwapo jina lako liko katika sajili ya uchaguzi wengi wamekuwa wakipiga nambari hizi *152*00#




About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top