MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim
Seif Sharif Hamad amesema matarajio yake makubwa kwamba Uchaguzi Mkuu
utakuwa huru na haki na yeye atakuwa wa kwanza kumpongeza atakayeshinda.
Maalim Seif aliyasema hayo huko Chake Chake Pemba katika uwanja wa Tibirinzi wakati akihutubia wananchi wa Pemba akihitimisha kampeni za uchaguzi katika kisiwa hicho. “Jumapili tunakwenda kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu...
Napenda kutamka bayana kwamba nikishindwa katika uchaguzi huru na haki nitampongeza aliyeshinda, lakini pia namtaka mwenzangu na yeye atamke hadharani kama mimi,” alisema Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF.
Aliitaja mikakati ya kuleta mabadiliko makubwa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyo nayo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa Muungano wa Serikali tatu ambao utaifanya Serikali ya Zanzibar kuwa na maamuzi kamili na mamlaka yake.
Alisema Wazanzibari kwa sasa wanataka kuona Zanzibar inakuwa nchi kamili yenye maamuzi yake pamoja na kuwa na muungano wenye maslahi ya pande zote mbili. “Nikichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar nitahakikisha kwamba naleta mabadiliko makubwa kwa Zanzibar ikiwemo kuwepo kwa Muungano wa Serikali tatu utakaoifanya Zanzibar kuwa dola kamili,” alisema.
Maalim alitangaza neema kwa wafanyakazi ikiwemo watumishi wa Serikali ambapo kima cha chini cha mshahara utakuwa Sh 400,000 huku askari wa vikosi vya SMZ wakilipwa Sh 450,000.
Aidha, alisema kiwango cha chini ya pensheni kwa wafanyakazi wastaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kitakuwa Sh 200,000 ili kuwawezesha watumishi waliolitumikia taifa hilo kuishi vizuri.
Mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya CUF alifunga kampeni za uchaguzi baada ya kufanya jumla ya mikutano 20 katika kisiwa cha Pemba ikiwemo mikutano ya ndani ya wanachama.

Post a Comment Blogger Facebook