![]() |
| Kirusi cha ebola |
Waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola
wametakiwa kutumia mipira ya kondomu hadi kutakapokuwa na ufahamu wa
kutosha kuhusu matokeo ya utafiti yanayoonyesha kwamba virusi hivyo
husalia katika majimaji ya mbegu za kiume kwa kipindi cha hadi miezi
tisa.
Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa maambukizi ya
ebola kupitia tendo la ngono ni kidogo mno na kutaja maeneo ya taifa la
Sierra Leone ambayo yana idadi kubwa ya manusura lakini hayana visa
vipya vinavyojirudia.Lakini mkuu wa WHO Margeret Chan ameiambia BBC kwamba kuna maswali mengi.''Hatujui iwapo wanaweza kuambukiza ama vipi ,bado hatuna ushahidi wa kutosha''.
''Kiwango cha ufahamu bado kinatutia wasiwasi ,ndio maana lazima tuchukue tahadhari ,kwa hivyo tunawashauri manusura kujilinda kupitia mipira''.

Post a Comment Blogger Facebook