Unknown Unknown Author
Title: Southampton 2- 3 Manchester United
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mshambulizi mpya wa Manchester United, Anthony Martial alithibitisha thamani yake alipoiongoza timu yake kusajili ushindi muhimu wa ma...
Mshambulizi mpya wa Manchester United, Anthony Martial alithibitisha thamani yake alipoiongoza timu yake kusajili ushindi muhimu wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya wenyeji wao Southampton.
Martial alijiunga the red devils kwa kitita cha pauni milioni 36 .
Man United walianza vibaya mechi hii na kuwaruhusu The saints kupata bao la mapema kupitia kwa Graziano Pelle.
Martial akimsaidia mpinzani wake Virgil van Dijk

Pelle alifuma kimiani mkwaju uliokuwa umetemwa na kipa wa United, David De Gea kunako dakika ya 13.
Hata hivyo Martial aliisawazishia United.
Martial hakukuwa amemalizana nao,
Mpira umekwisha na United wanarejea nyumbani na alama 3 muhimu

Alimpa kocha van Gaal sababu ya kutabasamu baada ya kutumia vyema makosa ya Maya Yoshida aliyemega mpira hafifu kurudi nyuma kwa mlinda lango naye akaufyatua kimiani.
Juan Mata alifunga bao la tatu dakika chache tu kabla ya Pelle kufunga bao lake na la pili na la Southampton.
Graziano Pellè anaifungia Southampton bao la pili
Vijana wa Louis van Gaal waliandikisha ushindi wao wa pili mfululizo baada ya kuibana Liverpool juma lililopita.
Kufuatia ushindi huo united wameimarika hadi kushika nafasi ya pili katika ligi ya EPL nyuma ya mahasimu wao manchester City.
Southampton imeshinda mechi mbili pekee baada ya kucheza mechi 12.
90:00 +5:20 Mpira umekwisha.
Southampton 2-3 Manchester United
Manchester United wanasajili ushindi muhimu dhidi ya Southampton





About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top