Rais wa bodi ya Kriket ya India
Jagmohan Dalmiya amefariki dunia. Dalmiya mwenye miaka 75 alifikishwa
hospitalini siku ya Alhamisi wiki iliyopita kutokana na maumivu ya kifua
huku akilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Amehudumu
katika nafasi ya Urais wa Kriket nchini humo tokea mwaka 2001 mpaka 2004
kwa kipindi cha mpito wa uongozi wa chama hicho ambapo alirudi tena
madaraani mwaka 2013 mpaka Machi 2015.Alikuwa pia kiongozi katika shirikisho la dunia la mchezo huotokea mwaka 1997 mpaka 2000.

Post a Comment Blogger Facebook