![]() |
| Kiongozi wa kidini wa Iran , Ayatollah Khamenei, ameitaka Saudi Arabia kuomba msamaha, kufuatia msongamano wa mahujaji huko Mecca |
Kiongozi wa kidini wa Iran ,
Ayatollah Khamenei, ameitaka Saudi Arabia kuomba msamaha, kufuatia
mauwaji ya msongamano wa mahujaji huko Mecca siku ya Alhamisi ambapo
zaidi ya watu 760 walifariki.
Taarifa hiyo iliyowekwa kwenye
mtandao wa kiongozi huyo wa kidini, inasema kuwa jamii ya kiislamu wana
maswali chungu nzima,badala ya kulaumu wengine.![]() |
| Zaidi ya raia 130 wa Iran walikuwa miongoni mwa waliofariki |
Saudi Arabia tayari imekatalia mbali ukosoaji kutoka kwa Iran kuhusiana na janga hilo na kuilaumu kwa kuingiza siasa katika mkasa huo mmbaya kuwahi kutokea kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Saudia, Adel al-Jubeir, ameishutumu Iran kwa kujaribu kuleta siasa katika mkasa huo uliwakumba watu ambao walikuwa wakitekeleza nguzo muhimu ya kidini.
Viongozi wa Iran wameelezea hasira zao kuhusiana na janga hilo huku wakiilaumu Saudi Arabia kwa kuongoza vibaya maeneo takatifu ya ibada kwa waislamu.
Zaidi ya raia 130 wa Iran walikuwa miongoni mwa waliofariki.


Post a Comment Blogger Facebook