![]() |
| Maalim Seif Sharif Hamad |
Mgombea urais wa Zanzibar kwa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ameeleza hayo wakati akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Kandwi jimbo la Chaani.
Alisema kwa muda mrefu wakulima wa mwani wamekuwa wakiishi maisha duni kutokana na bei ndogo ya zao hilo ikilinganishwa na gharama za uzalishaji, jambo aliloahidi kuwa serikali yake italipa umuhimu wa kipekee.
Maalim Seif alisema kama ilivyo kwa karafuu, Serikali atakayoiongoza itafanya utafiti wa bei ya mwani duniani, ili wakulima ambao wengi wao ni wanawake, waweze kunufaika ipasavyo na kilimo hicho.
Sambamba na hilo, Maalim Seif alisema iwapo atachaguliwa, Serikali yake itafanya utaratibu wa kulipa hadhi zao hilo hapahapa nchini, ili kuliongezea thamani yake katika soko la ndani na nje. “Tutawatoa wakulima kutumia jembe la mkono na kuendeleza kilimo cha kisasa”, alisisitiza.
Alisema pia wakulima watapatiwa utaalamu kuweza kulima mazao ya viungo yakiwemo tangawizi, ili kuepuka kuagizia mazao hayo kutoka Tanzania Bara. Katika hatua nyingine mgombea huyo wa urais kupitia CUF, alisema ataweka utawala wa sheria ili kila mtu aweze kupatiwa haki yake kwa mujibu wa sheria zilizopo.
“Hakuna atakayeonewa, kila mmoja atatendewa haki sawa na mwingine na wala hakuna atakayekuwa juu ya sheria”, alieleza. Kuhusu vitendo vya rushwa, aliahidi kupambana na vitendo hivyo kwa nguvu zake zote, kuweka maslahi mazuri kwa wafanyakazi ili Zanzibar iweze kuendelea bila ya rushwa na kwani imekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo.
Katika salamu zake kwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mwakilishi wa Viti Maalum anayemaliza muda wake kutoka Wilaya ya Kaskazini ‘A’, Kazija Kona, amewataka wanawake wa mkoa huo kumchagua Maalim Seif ili waondokane na kero ya kuwalipia ada kubwa ya shule watoto wao

Post a Comment Blogger Facebook