Unknown Unknown Author
Title: Auawa kwa kula kitoweo cha nyama India
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Nyama ya ngombe ni haramu maeneo mengi ya India ambapo Wahindu wanaamini mnyama huyo ni 'mtakatifu'. ...
Nyama ya ngombe ni haramu maeneo mengi ya India ambapo Wahindu wanaamini mnyama huyo ni 'mtakatifu'.
Polisi nchini India wamewatia mbaroni watu sita baada ya mwanamume mmoja Muislamu kupigwa hadi kufa kufuatia uvumi kuwa familia yake imeficha nyama nyumbani kwao.
Watu 6 wamekamatwa na polisi nchini India baada ya kumvamia na kumpiga mwanaume mmoja hadi kufa eti alikuwa amekula nyama ya ngombe.
Mohammed Akhlaq alikokotwa kutoka nyumbani kwake Kaskazini mwa Uttar Pradesh na kushambuliwa na umati wa watu.
Mwanawe pia alijeruhiwa vibaya.

Jamaa ya muathiriwa wakiomboleza kifo chake
Kuchinja ngombe ni haramu maeneo mengi ya India ambapo wakaazi wake wengi ni Wahindu wanaoamini mnyama huyo ni mtakatifu.
Hivi majuzi Serikali ya chama cha Wahindu chenye mrengo wa kulia kimeweka sheria kali zinazopiga marufuku uchinjaji wa ngombe, uuzaji wa nyama na ulaji wake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top